Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA jana tarehe 12/03/2019 imetoa msaada wa mafuta maalumu ya kuzuia madhara ya mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanaotoka kituo cha Albino Technical Service. Mafuta hayo yanasaidia watu wenye ualbino na athari zinazotokana na mionzi ya jua ikiwemo pamoja na salatani ya ngozi.
Msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi laki nane.
Akikabidhi msaada huo kwa miaba ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bi. Rehema Binamungu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Utahini na Utunuku alisema, licha ya kuwa mafuta hayo hayawezi kutosheleza mahitaji ya watu wenye ualbino kulingana na wingi wa uhitaji lakini msaada huo ni ishara ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA kuguswa na kundi hilo.
Bi. Binamungu alitumia fursa hiyo kuwashauri watu wenye ulemavu kuhamasishana katika kuangalia na kutumia fursa za mafunzo ya ufundi stadi ili kujiongezea ujuzi na kujikwamua kiuchumi.
“VETA tuna toa mafunzo ya aina mbalimbali yanayo lenga mahitaji ya makundi ya watu mbalimbali hivyo tunafursa sawa kwa kila mhitaji”
Kwa upande wake? mwakilishi wa kikundi cha Albino Technical Service Bi. Anna Luhoga aliishukuru VETA kwa msaada huo akisema kuwa wengi wa watu wenye ualbino hawana uwezo wa kununua mafuta hayo kwa kuwa yana bei kubwa.
”tunaishukuru VETA kwa kutupatia msaada huu kwa sababu mafuta haya yanauzwa kwa gharama kubwa na wengi wetu tunashindwa kuyanunua. Shughuli za watu wenye ulemavu wa ngozi mara nyingi ni za mikono, hali inayowapelekea muda mwingi kushinda juani hali inayosababisha kuharibika kwa ngozi zao, ” alisema.
Aliiomba VETA kuwasaidia watu wenye ulemavu katika masuala ya elimu ya ujasiriamali ili waweze kuongeza ujuzi katika kuendesha shughuli za kujiongezea kipato.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office