The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Utawala wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Ndg. Elifadhili Solomon, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, kwenye mahafali ya Chuo cha VETA Kihonda, yaliyofanyika tarehe 1 Disemba, 2023 ambapo wanafunzi 227 wamehitimu.
Ndg Solomon amesema TRC inathamini mafunzo ya ufundi stadi, kwani zaidi ya asilimia 60 ya watumishi wake ni mafundi wa aina mbalimbali.
Alitumia nafasi hiyo kuipongeza VETA kwa kutoa vijana wenye ujuzi ambao utalisaidia Taifa katika nyanja mbalimbali za ufundi stadi.
"Niwaase vijana mkatumie elimu mliyopewa kuisaidia jamii na pia kujiepusha na mambo mbalimbali yenye viashiria vya mmomonyoko wa maadili ili kuendelea kuwa na afya njema," amesema.
Aliwataka wazazi kuendelea kuwa karibu na vijana hao katika malezi ili waendelee kuwa na maadili mema na hivyo kuendelea kujenga taswira njema ya VETA popote watakapokwenda nchini.
Naye Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Mashariki, Ndugu Wilhard Soko, ameziomba taasisi zilizoshiriki katika mahafali hayo kutoa kipaumbele kwa vijana waliohitimu VETA wakati wanapoajiri.
" Nimeona waajiri wengi mpo hapa, nimewaona Agricom, TRC, Alliance one, TANESCO , MOROWASA, na Benki mbalimbali. Rai yangu kwenu wasaidieni vijana hawa, wana weledi na ufundi wa kutosha na wenye kuleta matokeo," amesisitiza ndugu Soko.
Ndugu Soko amewasihi wahitimu hao kuwa mabalozi wema wa VETA kwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa waaminifu na kupenda kazi nyakati zote wawapo kazini.
Naye, Mkuu wa chuo cha VETA Kihonda, Bi. Theresia Ibrahim, amesema wahitimu hao ni wa fani za Ufundi Uashi; Ushonaji; Ubunifu wa Mavazi na Teknolojia ya Nguo; Useremala; Ufundi Majokofu na Viyoyozi; umeme wa majumbani; Ufundi Mitambo na Ukerezaji Vyuma; Ufundi Magari na Umeme wa Magari.
Aidha, Bi Theresia amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuendelea kushirikiana na chuo hicho katika kutoa mafunzo stadi na kuongeza kuwa chuo kinajivunia na kuthamini ushirikiano huo.