The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
WAZIRI MKUU AIPONGEZA VETA KWA BUNIFU ZENYE TIJA KWA JAMII
Posted on: Sunday, 02 June 2024
WAZIRI MKUU AIPONGEZA VETA KWA BUNIFU ZENYE TIJA KWA JAMII
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb) ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa ubunifu unaolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Mhe. Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la VETA, leo tarehe 31 Mei 2024, katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal, jijini Tanga.
Akiwa katika banda hilo la VETA Waziri Mkuu Majaliwa, alijiionea ubunifu wa kifaa cha kuongeza usikivu kwa watu wenye usikivu hafifu na kifaa cha kudhibiti dereva kusinzia wakati akiendesha gari.
"Tumekuwa na watu wengi wanaosumbuliwa na tatizo la usikivu hafifu ambapo tukiwatumia VETA na wabunifu wao tunaweza kuzalisha vifaa vingi na vya kutosha ndani ya nchi vitakavyowasaidia badala ya kuagiza kutoka nje" amesema.
Naye ndugu Innocent Maziku, Mwalimu na mbunifu wa kifaa hicho cha kuongeza usikivu kwa watu wenye usikivu hafifu kutoka chuo cha VETA Kigoma ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mamlaka husika katika kusaidia kuzalishwa/kutengenezwa kwa vifaa hivyo kwa wingi ili kuwasaidia Watanzania wengi wenye tatizo hilo.
Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza rasmi tarehe 25 Mei, 2024 yamekifia kilele na kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 31 Mei, 2024