The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Waziri Ndejembi afurahishwa na mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wenye mahitaji maalum
Posted on: Wednesday, 10 July 2024
Waziri Ndejembi afurahishwa na mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wenye mahitaji maalum yanayotolewa na VETA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, ameeleza kufurahishwa kwake na umahiri wa watu wenye mahitaji maalum baada ya kupata mafunzo VETA.
Mhe. Ndejembi amesema hayo leo tarehe 7 Julai, 2024 alipotembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na kujionea kazi zinazofanywa na wanafunzi na wahitimu wa VETA wenye mahitaji maalum.
Ametoa pongezi kwa VETA kwa kutoa mafunzo kwa kundi hilo maalum na kuahidi kufanya ziara VETA ili kujionea kwa kina namna mafunzo hayo yanavyotolewa na kushirikiana na VETA kuweka mikakati itakayowezesha mafunzo hayo kuwafikia wahitaji wengi zaidi.
“Nimefurahishwa sana na hii programu ya VETA ya kutoa mafunzo ya ufundi stadi jwa watu wenye mahitaji maalum… nawapongeza sana kwa hatua hii na ninaahidi kuwatembelea ili kujadiliana nanyi namna tunavyoweza kuwafikoa watu wengi zaidi wenye mahitaji maalum,” amesema
Mhe. Ndejembi pia ameahidi kumtembelea Ndg. Boniface Kiyenze, mhitimu wa VETA wa fani ya Useremala mwenye mahitaji maalum aliyejiajiri katika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam.