MAKISATU 2021
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawaalika Watanzania wenye Ubunifu, Ugunduzi na Maarifa Asilia kushiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa mwaka 2021.
Usajili utaanza tarehe 18 Novemba 2020 hadi tarehe 18 Januari 2021
Mwongozo wa fomu za usajili zinapatikana kupitia wavuti www.makisatu.costech.or.tz. au Bonyeza hapa
VETA inaratibu usajili wa makundi ya Vyuo vya Ufundi Stadi na Mfumo Usio Rasmi. Taarifa kuhusu mashindano hayo pia zinapatikana kwenye tovuti ya www.veta.go.tz.
Watanzania wenye Ubunifu, Ugunduzi na Maarifa Asilia waliopo katika Vyuo vya Ufundi Stadi na Mfumo usio Rasmi wawasilishe maombi yao kupitia info@veta.go.tz, au pr@veta.go.tz au makisatu@moe.go.tz au kuwasilisha kwa mkono kwenye ofisi za VETA katika mikoa na wilaya zilizo karibu nao.
Tathmini ya ubunifu uliowasilishwa itafanyika ili kupata washindi watakaoshiriki katika kilele cha MAKISATU 2021.
Kwa mawasiliano na taarifa zaidi:
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), S. L. P. 2849, Dar es Salaam Simu: 0767 920 019 au 0754 868 689 au 0754 520 176 au 0784 865 994
“SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KWA UCHUMI ENDELEVU”
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office